Waziri wa Fedha Kitui aponea kung’atuliwa na bunge

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Fedha wa serikali ya kaunti ya Kitui Peter Kilonzo ameponea chupuchupu kung’atuliwa afisini na bunge la kaunti hiyo, baada ya jaribio la kumbandua kushindwa kufua dafu.

Hoja ya kumbandua madarakani haikupata uungwaji mkono wa kutosha katika bunge huku spika Kelvin Kinengo akilazimika kuifutilia mbali.

Aidha, baadhi ya wawakilishi wadi wameombwa kushikana mkono na upande wa serikali ili kutekeleza maendeleo kwenye kaunti hiyo.

Akizungumza baada ya kunusurika, Kilonzo amewashutumu waliowasilisha hoja ya kumbandua akisema kuwa maswala yaliyoibuliwa yalikuwa ya usimamizi na ya kujadiliwa wala hayakuhitaji kufika bungeni.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *