Waziri Machogu kutangaza matokeo ya mtihani wa CBET

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu siku ya Alhamisi anatarajiwa kutangaza matokeo ya mtihani wa elimu ya umilisi kwa wakufunzi, Competency-Based Education and Training maarufu kama CBET ambayo yamesubiriwa kwa muda mrefu.

Machogu ataongoza utoaji wa hati za mtihani huo pamoja na vyeti kwa waliotahiniwa baina ya mwezi Novemba na Disemba mwaka uliopita.

Matokeo hayo yatakuwa ya kwanza kutangazwa tangu kuanzishwa kwa CBET mwaka 2019.

Hafla hiyo itaandalia katika chuo cha TVET cha Gigiri.

Share This Article