Waziri wa Habari Teknoljia Mawasiliano na Uchumi wa kidijitali Eliud Owalo na Katibu katika wizara ya usalama wa taifa Dkt Raymond Omollo,wamefanya mashauriano katika kaunti ya Kisumu siku ya Jumapili na wasomi wengine kutoka kaunti hiyo kabla ya ziara ya Rais William Ruto baadae wiki hii.
Omollo amesema kuwa Rais atazindua miradi mbali mbali ya kitaifa wakati wa ziara hiyo katika kaunti za Kisumu, Siaya, Homabay na Migori .
Akiwa Kisumu Ruto atazuru kituo cha mabilioni ya pesa cha utafiti wa samaki cha Kabonyo Kanyagwal huko Nyando.
Kulingana na katibu Omollo Rais pia atakagua ujenzi wa barabara ya Muhoroni na jumba la Lake Basin Development Authority (LBDA) lililo barabara kuu ya Kisumu -Kakamega miongoni mwa miradi mingine.
Katika kaunti ya Homabay Ruto atakagua ujenzi wa barabara ya Mfangano ring na ile ya Mbita-Sindo-Magunga.
Kwenye kaunti ya Migori, Rais atawatembelea wakulima wa miwa na wanafunzi wa chuo kikuu Rongo.
Katika kaunti ya Siaya Ruto atazuru taasisi za kutoa mafunzo ya kiufundi maeneo ya Gem , Rarieda na Bondo, kabla ya kuzindua ujenzi wa barabara ya Bondo-Liunda.
Kulingana na Omollo Rais Ruto, anatarajiwa kukutana na voingozi wa eneo hilo la Nyanza