Waziri Owalo ateuliwa kwa bodi ya ITU

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Eliud Owalo ameteuliwa kuwa mwanachama wa Bodi ya Uvumbuzi wa Dijitali Duniani ya Umoja wa Mawasiliano Duniani, ITU.

Bodi ya Uvumbuzi wa Dijitali Duniani huchangia uvumbuzi kwa kiwango kikubwa na hulenga kusawazisha uvumbuzi miongoni mwa mataifa wanachama.

Owalo ni miongoni mwa maafisa 18 kutoka mataifa mbalimbali walioteuliwa kuwa wanachama wa bodi hiyo.

Akizungumza baada ya uteuzi huo, Waziri Owalo alisema kuwa serikali Kenya inatambua na kutoa kipaumbele kwa teknolojia ya habari na mawasiliano, ambayo ni kichocheo muhimu kwa ukuaji wa maendeleo kupitia kwa mfumo wa serikali wa kuanzia chini kwenda juu.

“Ajenda yetu ya kuleta mabadiliko kupitia dijitali inahusisha miundombinu mwafaka na thabiti kupitia uwezeshaji wa maarifa ya ajira za mitandaoni, kuwaunganisha watu kupitia kwa mtandao wa Wi-Fi na kubuni mazingira bora ya kufanya biashara za mtandaoni kupitia kupunguza uhalifu wa mitandaoni,” alisema Owalo.

Website |  + posts
Share This Article