Waziri Owalo aongoza utiaji saini wa kandarasi za utendakazi

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali Eliud Owalo ameongoza shughuli ya utiaji saini kandarasi za utendakazi kwa maafisa wa wizara yake.

Waziri Owalo ameongoza mchakato huo siku ya Jumatatu, katika makao makuu ya wizara akiwahimiza maafisa hao kutekeleza wajibu wao ipasavyo kulingana na kandarasi.

Maafisa waliosaini mikataba ya utendakazi ni pamoja na makatibu, wenyeviti na maafisa wakuu watendaji wizarani.

Waziri Owalo alikariri kujitolea kwa wizara yake kuliongoza taifa kuhamishia shughuli na huduma zote za serikali mtandoani kuambatana na ajenda ya mfumo wa kiuchumi wa serikali ya Kenya Kwanza wa kuanzia chini kuelekea juu.

Share This Article