Waziri wa mawasiliano na uchumi dijitali Eliud Owalo kupitia kwa wakfu wake, ameanzisha shindano la mchezo wa soka katika eneo ambalo awali lilifahamika kama mkoa wa Nyanza.
Shindano hilo kwa jina “ELIUD OWALO SUPER CUP TOURNAMENT 2023” litakuwa la siku 5 kati ya Disemba 26 na 30 2023.
Kulingana na taarifa ya kutangaza ujio wa shindano hilo, lengo lake ni kuboresha viwango vya mchezo wa soka kati ya vijana katika kaunti za Migori, Homabay, Kisumu na Siaya.
Litasaidia kuepusha vijana na matatizo kama matumizi ya dawa za kulevya na pombe na kuwasaidia pia kujipatia riziki kupitia talanta ya soka.
Kando na shindano hili, wakfu wa Eliud Owalo umekuwa ukisaidia timu mbali mbali kama Gor Mahia ambayo ilinunuliwa basi la kisasa kwa ajili ya usafiri na usaidizi wa kifedha na vifaa kwa timu kama AFC Leopards SC, Migori Youth FC, Shabana F na Muhoroni Youth FC.
Wakfu huo unashirikiana na kundi la soka ya vijana la Winam ambalo wanachama wake ni pamoja na James Goro Oronge, Tobias Ochola ‘Juakali,’ Peter Dawo na Gerald Omollo ‘Chonjo’ katika maandalizi ya shindano hilo.
Tazama ratiba ya shindano hilo hapa;
MATCH DAY 1
DATE: 26/12/2023
TEAMS: Homabay Combined vs Migori Combined
KICK OFF: 3:00PM
VENUE: Raila Odinga Stadium, Homabay
ENTRANCE: FREE
MATCH DAY 2
DATE: 27/12/2023
TEAMS: Kisumu Combined vs Siaya Combined
VENUE: Jomo Kenyatta International Stadium, Mamboleo Kisumu
KICK OFF: 3:00PM
ENTRANCE: FREE
MATCH DAY 3
DATE: 28/12/23
Match A
TEAMS: (3rd place play-off) Loser Match Day 1 vs Loser Match Day 2
VENUE: Jomo Kenyatta International Stadium, Mamboleo Kisumu
KICK OFF: 12 NOON
ENTRANCE: FREE
Match B: Final
TEAMS: Winner Match Day 1 vs Winner Match Day 2
VENUE: Jomo Kenyatta International Stadium, Mamboleo Kisumu
KICK OFF: 3:00PM
ENTRANCE: FREE
MATCH DAY 4
DATE: 30/12/23
TEAMS: Nyanza Combined vs Gor Mahia
VENUE: Nyilima Grounds, Asembo, Rarieda
KICK OFF: 3:00PM
ENTRANCE: FREE