Waziri Nakhumicha atoa shilingi milioni 17 kwa watoa huduma ya afya jamii kote nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa afya Susan Nakhumicha ametoa shilingi milioni 17 kuwalipa wastawishaji wa afya ya jamii kote nchini.

Waziri akiwa katika hafla moja katika kaunti ya Bungoma amesema pesa hizo zitatumika kulipia marupuru ya maafisa hao katika miezi ya Disemba na Januari.

Jumla ya wastawishaji wa afya ya jamii 3500 kote nchini watapokea malipo ya shilingi 5,000 kila mmoja.

Haya yanajiri wiki moja tu baada ya serikali kutoa shilingi bilioni 3 kuwagharamia wastawishaji wa afya ya jamii.

Share This Article