Waziri wa Utalii Dkt. Alfred Mutua kwa yupo nchini Rwanda anakohudhuria Kongamano la Baraza la Usafiri na Utalii Duniani.
Hii ni mara ya kwanza kwa kongamano hilo kuandaliwa katika nchi ya bara la Afrika.
“Wakati wa kongamano hilo, tulishiriki majadiliano muhimu kuhusu namna ya kuwezesha usafiri usiokuwa na vikwazo wa watalii barani Afrika, hasa kwa kuangazia uboreshaji wa uchukuzi wa anga na reli,” amesema Dkt. Mutua.
Inakadiriwa kuwa sekta ya utalii itakua kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 5 mwaka ujao, na yamkini kubuni nafasi zaidi ya milioni 6 za ajira.
“Ili kufikia ukuaji huu. lengo letu kuu ni kujiandaa kimkakati kwa kuongeza juhudi za kuinadi nchi hii na kuongeza vituo vya kitalii hasa katika nyanja za utalii wa michezo na kujionea maeneo mbalimbali,” aliongeza Dkt. Mutua.