Waziri wa Michezo Kipchumba Murkomen amesema kuwa ukarabati unaoendelea katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani, na wanajeshi utakamilika Novemba 30 mwaka huu na kuanza kutumika Disemba mosi.
Murkomen alisema haya Ijumaa alipofanya ziara ya kukagua viwanja nchini nchini ,huku Kenya ikitarajiwa kuandaa fainali za CHAN mwaka ujao na AFCON mwaka 2027.
Waziri pia alisema atachapisha hivi karibuni vigezo vya kuongoza ujenzi wa viwanja nchini vya sirikali kuu,serikali za kaunti na pia wastawishaji wa kibinafsi wanaoekeza katika kujenga viwanja.
Kulingana na waziri hali hii itahakikisha viwanja vyote vinaafiki viwango vya kimataifa kuandaa mechi na mashindano.
Pia uwanja wa Nyayo unakarabatiwa huku pia kukiwa na ujenzi wa uchanjaa wa Talanta City Sports unaotarajiwa kuselehi mashabiki 60,000,utakapokamilika.