Waziri Mkuu wa Tunisia Kamel Madouri apigwa kalamu

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Tunisia Kais Saied amemtimua Waziri Mkuu wake Kamel Madouri, mapema leo huku joto la kisiasa.

Madouri, aliyeteuliwa Agosti mwaka jana amefurushwa huku nafasi ikitwaliwa na Sarra Zaafrani Zenzrika katika badiliko pekee la serikali.

Hata hivyo serikali haijatoa sababu za kumtimua Madouri.

Zaafrani,aliye na umri miaka 62,ndiye mwanamke wa pili kuhudumu serikali katika wadhfa huo baada ya Najla Bouden,aliyehudumu kati ya mwaka 2021 hadi 2023.

Tunisia,inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi,ukosefu wa ajira na madeni.

Website |  + posts
Share This Article