Waziri Mkuu wa Nepal Sharma Oli ajiuzulu huku waandamanaji wakitekeza bunge

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri Mkuu wa Nepal Sharma Oli aliyejiuzulu

Waziri Mkuu wa Nepal Sharma Oli, amejiuzulu huku maandamano yakichacha kufuatIa kuuawa kwa waandamanaji 19, waliokuwa wakikabiliana na polisi Jumatatu.

Maelfu ya waandamanaji siku ya Jumanne waliteketeza bunge lililo katika mji mkuu Kathmandu, huku majengo mengine pia yakiteketezwa.

Wandamanaji wanne waliripotiwa kuuawa jana Jumanne huku pia wafungwa 900 wakitoroka gerezani.

Waandamanaji hao walianza kwa kupinga hatua ya serikali kufunga mitandao yote ya kijamii, na maandamano yakaendelea licha ya serikali kuondoa vikwazo.

Licha ya kujiuzulu kwa Waziri huyo Mkuu, maandamano yameendelea huku waandamanaji wakivunja na kuingia bungeni na kuliteketeza.

 

Website |  + posts
Share This Article