Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alazwa hospitalini

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelazwa hospitalini ili kupata huduma ya dharura ya kuwekewa kifaa cha kusaidia kuongeza kasi ya moyo kupiga.

Haya yanajiri kabla ya kura muhimu bungeni kuhusu mpango wake wa kufanya mabadiliko kwenye idara ya mahakama.

Amelazwa katika hospitali ya Sheba huko Tel HaShomer.

Afisi ya waziri mkuu nchini Israel ilitoa taarifa leo kwamba kiongozi huyo wa umri wa miaka 73 atatulizwa kwa dawa na hivyo waziri wa masuala ya haki Yariv Levin, atamkaimu.

Kwenye ujumbe wa video, Netanyahu naye alisema kwamba anajihisi vyema na ataendeleza mpango wake punde baada ya kuondoka hospitalini.

Ujumbe huo wa usiku wa manane ulijiri wiki moja baada ya Netanyahu kulazwa hospitalini kwa kile kilichotajwa kuwa kukosa maji mwilini, na baada ya siku ya maandamano makubwa ya walio kinyume na mpango wake wa kuibadilisha kabisa idara ya mahakama.

Jumamosi waandamanaji walijaa kwenye barabara za miji nchini Israel huku wengi wakiingia Jerusalem na kupiga kambi nje ya bunge kabla ya kura bungeni humo, kuhusu nia hiyo ya Netanyahu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *