Waziri Mkuu wa Haiti kuzuru Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry anatarajiwa kuzuru nchini Kenya hivi karibuni katika harakati za kutafuta suluhisho la kutumwa kwa polisi wa Kenya katika nchi hiyo ya Caribbean kudumisha usalama.

Kulingana na taarifa, Henry anatarajiwa kuhudhuria kikao cha 46 cha muungano wa mataifa ya eneo la Caribbean (Caricom) kitakachoandaliwa nchini Guyana, kabla ya kuzuru Kenya.

Serikali ya Kenya inapanga kutuma polisi 1,000 wakiwemo wa vitengo vya Rapid Deployment-RDU, vile vya kupamana na wizi wa mifugo, vya kushika doria mpakani na GSU.

Wakati wa ziara yake nchini Kenya, Waziri Mkuu huyo anatarajiwa kutia saini makubaliano kati ya Kenya na Haiti, kabla ya polisi kutumwa kutoka Kenya.

Benin pia inatarajiwa kutuma polisi wengine 2,000 nchini Haiti kusaidia udumishaji usalama.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article