Trump alaani mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine

Tom Mathinji and BBC
1 Min Read
Rais wa Marekani Donald Trump.

Rais wa Marekani Donald Trump amelaani mashambulizi ya Urusi yaliyotekelezwa nchini Ukraine.

Kupitia mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema hakufurahishwa na mashambulizi ya Urusi huko Kyiv.

“Hakuna haja ya kufanya hivyo, na huu ni wakati mbaya. Vladimir, Acha! Wanajeshi 5000 wanakufa kwa wiki. Makubaliano ya amani yaafikiwe,” alisema Trump.

Wizara ya ulinzi ya Urusi inadai kuwa mashambulizi hayo yalilenga “usafiri wa anga, roketi na anga, makampuni ya ujenzi wa mashine na viwanda vya vifaru nchini Ukraine, makampuni yanayozalisha mafuta ya roketi na baruti”.

“Maeneo lengwa ya shambulizi hilo yamefikiwa. Yote yameshambuliwa,” wizara ya ulinzi ilisema katika taarifa.

Ujumbe wa Trump umejitokeza saa chache baada ya Trump kumkosoa rais wa Ukraine kwenye jukwaa hilo hilo.

“Yeye [Zelensky] anaweza kuwa na amani au, anaweza kupigana kwa miaka mingine mitatu kabla ya kupoteza nchi nzima,” Trump aliandika Jumatano, akiongeza kuwa Zelensky ndiye “asiye na chaguo la kumwezesha kufanikiwa”.

Ujumbe wa Trump kwa Putin ni nadra sana kulaani mashambulizi ya kila siku ya Urusi dhidi ya Ukraine – na ishara ya kufadhaika kwake.

Website |  + posts
Share This Article