Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille afutwa kazi

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille aondolewa mamlakani.

Baraza la mpito nchini Haiti limemfuta kazi kaimu Waziri Mkuu Garry Conille, miezi sita baada ya kuongoza taifa hilo la Caribbean.

Kulingana na amri ya utendaji iliyotiwa saini na wanachama wanane kati ya tisa wa baraza hilo, nafasi ya Conille ilichukuliwa na mfanyabiashara Alix Didier Fils-Aime.

Baraza hilo lenye wanachama tisa, ambalo lilibuniwa mwezi Aprili kutatua mzozo nchini humo, lilimchagua Conille May 3, 2024 kwenye wadhifa huo.

Hata hivyo, Conille amepinga kuondolewa kwake mamlakani akitaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria, akisema,” hatua hiyo iliibua wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa Haiti”.

Kenya imewatuma maafisa 600 wa polisi nchini Haiti kukabiliana na magenge yanayowahangaisha raia wa nchi hiyo, huku maafisa wengine 300 wa polisi wakijiandaa kuelekea nchini humo.

Kenya imejukumiwa na kuongoza mchakato wa kuleta amani nchini Haiti.

Watu zaidi ya 3,600 wameuawa nchini Haiti tangu Januari na zaidi ya 500,000 wamelazimika kuondoka makwao, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa.

Share This Article