Mtihani wa kitaifa wa utathmini wa gredi ya sita KPSEA unaanza leo asubuhi na unahusisha wanafunzi milioni 1.3 waliosajiliwa.
Waziri wa elimu Julius Migos Ogamba alisimamia shughuli ya kusambaza karatasi za mtihani huo, kutoka kwenye kasha la baraza la mitihani nchini KNEC lililoko kwenye afisi ya naibu kamishna wa kaunti eneo la Westlands kaunti ya Nairobi.
Ogamba vile vile ametangaza kubuniwa kwa jopo linalojumuisha maafisa wa wizara ya elimu na wale wa wizara ya mambo ya ndani linalijukumiwa kuhakikisha mtihani huo unafanyika vyema.
Awali akiwa katika kaunti ya Kisii, waziri huyo alitangaza kwamba kuna mipango ya kuhakikisha maandalizi ya vikao maalumu vya mahakama vya kushughulikia kesi zitakazoibuka za udanganyifu kwenye mitihani ya kitaifa.
Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE nao unaendelea kote nchini na unahusisha watahiniwa wapatao laki 9.