Waziri Mbadi aongoza ujumbe wa Kenya kwenye mkutano wa IMF Marekani

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri wa Fedha John Mbadi, anaongoza ujumbe wa ngazi ya juu kwenye Mikutano ya Mwaka ya shirika la fedha duniani, IMF na Benki ya Dunia ya mwaka 2024 inayoandaliwa Washington, D.C., Marekani.

Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kufanikisha kwa juhudi” ikiangazia ufufuzi wa uchumi unaoendelea nchini unaoonekana kupitia kushuka kwa mfumuko wa bei, kiwango cha ubadilishaji cha fedha na ukuaji thabiti wa Pato jumla la Taifa (GDP).

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) Kamau Thugge, Katibu Chris Kiptoo miongoni mwa maafisa wengine wakuu kutoka taasisi zote mbili ni sehemu ya kundi la maafisa walioandamana naye.

Kulingana na wMikutano hiyo itatumika kama jukwaa muhimu kwa wajumbe hao kuwasiliana na viongozi wa kimataifa kuhusu masuala ya dharura ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na uthabiti wa kifedha, kupunguza umaskini, na maendeleo endelevu.

Mikutano ya Mwaka huu ya IMF na Benki ya Dunia inatoa jukwaa la kimataifa kwa Kenya kuimarisha ushirikiano wake wa kimataifa na kupanda jukwaa na kuongoza katika ramani ya maendeleo endelevu.

Mikutano hiyo iliyoanza Jumatatu itakamilika Jumamosi.

TAGGED:
Share This Article