Waziri Linturi: Tunafanya mipango ya kuhakikisha wakulima wanapokea mbolea kwa urahisi

Martin Mwanje
1 Min Read

Waziri wa Kilimo Mithika Linturi amesema wizara yake inafanya mipango ya kuhakikisha mbolea ya bei nafuu inayotolewa na serikali inapelekwa karibu na vituo vilivyo karibu na wakulima. 

Mithika amesema wizara yake inafanya kazi na serikali za kaunti kuhakikisha hilo linatimia.

Alikuwa akimjibu Rais William Ruto aliyetaka kujua hatua wizara inachukua kuangazia suala hilo kufuatia malalamiko ya wakulima kwamba wanalazimika kusafiri mwendo mrefu ili kuipata mbolea hiyo.

Kwa sasa, wakulima wengi wanalizimika kusafiri hadi kwenye maghala ya Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao, NCPB ili kuchukua mbolea walioagiza.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya GavaMkononi inayotoa huduma za serikali kwa njia ya mtandao, Mithika alisema wizara yake tayari imeweka huduma 936 kwenye programu hiyo.

Alisema huduma zingine 3,500 zitawekwa kwenye programu hiyo katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Jumla ya huduma 5,000 tayari zimewekwa kwenye programu hiyo huku serikali ikilenga kuweka huduma zake zote kwenye programu hiyo.

Lengo ni kuboresha utoaji huduma kwa Wakenya na pia ukusanyaji ushuru kwa kuziba mianya ya ufisadi.

Website |  + posts
Share This Article