Waziri Linturi ajibu maswali katika bunge la seneti

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri wa kilimo Mithika Linturi, alifika katika bunge la seneti kujibu maswali mbali mbali yaliyoibuliwa na maseneta na ambayo yanahusu wizara yake.

Seneta Joyce Korir alitaka kujua mikakati iliyowekwa na serikali kudhibiti nyama isiyofaa ambayo inauziwa wakenya.

Linturi alijibu akisema kwamba serikali imebuni sera ya kutibu magonjwa ya mifugo na kudhibiti usafirishaji wa nyama kutoka vichinjio hadi kwa wauzaji. vile vile alisema kwamba taasisi za mafunzo ya nyama pia zinafanikisha elimu ya kuhakiki nyama nzuri na salama Kwa matumizi.

Seneta James Murango naye alitaka kujua ni vipi serikali inahakikisha kahawa na bidhaa za kahawa zinaafikia viwango vilivyowekwa na muungano wa Ulaya kuhusu kahawa na udhibiti wa ukataji wa miti-EUDR.

Waziri alijibu kuwa, wizara ya kilimo na ufugaji, mashiririka ya serikali kuu na serikali za kaunti, zinashirikiana kukusanya maeneo kijografia Kwenye mashamba ya kahawa na kisha kudadisi habari hizo Kwa kutumia mtambo wa GPS na setilaiti. Pia inabuni kituo cha njia ICT kitakachoonyesha njia za kidijitali za kahawa na kuweka taarifa za kilimo hicho.

Waziri pia aliangazia mafuriko ya hivi maajuzi kwenye kaunti ya Tana River na kusema kuwa mifugo, mimea na masoko yaliathirika ila serikali imetoa usaidizi Kwa walioathirika.

Share This Article