Waziri Kagwe aweka mikakati ya kulainisha sekta ya chai nchini

Dismas Otuke
2 Min Read

Waziri wa Kilimo na Ustawishaji wa Mifugo Mutahi Kagwe jana Alhamisi alifanya kikao na wadau wa sekta ya kilimo cha chai nchini kubaini changamoto zinazokabili sekta hiyo kwa jumla na kuweka mikakati mwafaka ya kulainisha sekta hiyo.

Kagwe alikutana na Shirika la Ustawishaji Chai nchini (KTDA), Chama cha Wakuza Chai (KTGA), Chama cha Wakuza Chai wa Kibinafsi (ITP), na Chama cha Wakuza Chai Afrika Mashariki (EATTA).

Baadhi ya maafikiano kwenye kikao hicho nia pamoja na;

1. Wadau wote wa chai waweke kipaumbele kuongeza tija kwa mkulima wa chai, kutekeleza shughuli zao kwa uwazi na uadilifu na usimamizi bora.

2. Wakuza chai wote ni sharti wazingatie sheria zitakazowekwa kuzuia uchumaji haramu wa chai, huku wadau wote watakaokiuka wakipokonywa leseni na halmashauri ya chai nchini – KTB.

3. Wazalishaji wote wa chai watekeleze sheria za kuongeza thamani ya viwango vya chai inayozalishwa nchini.

4. Serikali kuimarisha masoko ya chai kupitia uhamasishaji wa masoko ya chai humu nchini na kimataifa.

5. Serikali kubuni mikakati ya kuwalinda wawekezaji katika sekta ya chai na biashara ya kuongeza thamani.

6. EATTA kuweka mikakati ya kurejesha minada ya kuuza chai itakayofikiwa kiurahisi na wanunuzi na wauzaji chai duniani.

7. Serikali kushirikisha diplomasia katika mataifa ya Iran na Sudan ili kupanua masoko hayo ya chai.

8. Serikali kuhimiza uongezaji thamani chai ya humu nchini pamoja na kuweka sheria za kuondoa ushuru unaotozwa bidhaa za kupakia chai.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *