Waziri Duale kuhudhuria mkutano kuhusu Mazingira Ivory Coast

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Mazingira Aden Duale.

Waziri wa mazingira Aden Duale, Jumatano asubuhi aliondoka hapa nchini kuelekea Abidjan, Ivory Coast, kuiwakilisha Kenya kwa kongamano la 10 la Mawaziri kuhusu Mazingira (AMCEN), litakaloandaliwa Septemba 5 na 6, 2024.

Kongamano la AMCEN ni jukwaa la Mawaziri wa bara Afrika, kujadili na kubuni mikakati kuhusu maswala yanayoathiri mazingira katika bara hili.

Mkutano wa mwaka huu ni muhimu sana, kwa kuwa unalenga kushughulikia changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi, ukataji wa miti na hasara itokanayo na bio anuwai, huku wakitoa suluhu zitakazofaidi mataifa ya Afrika.

Matokeo ya mkutano huo, yanalenga kutoa mwongozo kuhusu sera za mazingira na mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi duniani.

Kenya, ambayo inatambulika kwa juhudi zake za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, inatarajiwa kuelezea mikakati yake ikiwa ni pamoja na mpango wa kitaifa wa upanzi wa miti bilioni 15, unaolenga kuongeza utandu wa misitu kufikia asilimia 30.

Share This Article