Waziri Ababu ahudhuria seminaa ya 40 ya mashirikisho ya Olimpiki Afrika-ANOCA

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amehudhuria seminaa ya 40 ya muungano wa mashirikisho ya Olimpiki barani Afrika,ANOCA siku ya Jumamosi .

Kikao hicho kimejadili kwa mapana matayarisho ya timu za Afrika, zitakazoshiriki makala ya mwaka ujao ya michezo ya Olimpiki jijini Paris Ufaransa.

Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa kwenye seminaa ni maandalizi kuhusu kambi ya timu za Afrika,usafari wao na kuwasili katika kijiji cha wanariadha jijini Paris.

Rais wa Kamati ya Olimpiki Kenya Paul Tergat akihutubia kikao

Maafisa waliohudhuria seminaa hiyo ni pamoja na katibu mkuu wa shirikisho la Olimpiki Afrika-ANOCA Ahmed Abou Elgasim Hashim ,Rais wa kamati ya Olimpiki nchini, ambaye pia ni mwanachama wa ANOCA, Paul Tergat na mwanachma wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC Kipchoge Keino.

Waziri Ababu akihutubu amewakaribisha wanachama wote 54 wa ANOCA wanaohudhiria seminaa hiyo na kuipongeza NOC-K kwa kupata fursa adimu kuandaa kikao hicho.

Waziri alikariri kuwa serikali itaiunga mkono kwa hali mali timu ya Kenya inapojiandaa kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao kuhakikisha inafanya vyema.

Share This Article