Wawakilishi wadi Kericho wamtimua katibu wa kaunti

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu wa kaunti ya Kericho Dkt. Wesley Bor aliyetimuliwa.

Wawakilishi wadi katika kaunti ya Kericho wamepitisha kwa kauli moja hoja ya kumtimua katibu wa kaunti hiyo Dr. Wesley Bor kwa madai ya ukiukaji wa katiba na utendakazi duni.

Kulingana na Paul Bii ambaye ni mwakilishi wadi ya Kapsaos aliyewasilisha hoja hiyo, wamekuwa wakichunguza mienendo ya katibu huyo kufuatia malalamishi ya wananchi na wafanyikazi wa serikali ya kaunti hiyo.

Bii alisema baadhi ya madai yaliotolewa dhidi ya katibu huyo ni kuhamishwa kiholela kuwa wafanyikazi wa kaunti hiyo bila kuzingatia sheria na kanuni zilizoko.

Mwakilishi wa wodi ya Ainamoi Cheruiyot Bett alisema Bor  pia alihusishwa na matumizi mabaya ya shilingi milioni  39 zilizotengewa mpango wa Kazi Mtaani.

Alidai pesa hizo zilitoweka kupitia baadhi ya kampuni zinazohusiana na katibu huyo.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *