Wavuvi wataka usalama kuimarishwa katika Ziwa Victoria

Tom Mathinji
1 Min Read

Wavuvi katika Ziwa Victoria wameiomba serikali kutumia bajeti iliyotengwa kwa ajili ya uchumi wa baharini na uvuvi ili kuimarisha usalama katika Ziwa Victoria.

Wavuvi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Muungano wa makundi ya Usimamizi wa fuo za bahari katika Kaunti ya Homa Bay, Edward Oremo, walisema kuwa shilingi bilioni 118 zilizotengewa sekta hiyo zinafaa kutumiwa kwa busara ili kuchochea ukuaji wa uchumi katika kaunti hiyo.

Aliitaka serikali kutumia fedha zilizotengwa sekta ya uvuvi katika kukabiliana na ukosefu wa usalama kwenye Ziwa Victoria.

Oremo pia aliiomba serikali kutoa ruzuku kwa vifaa vya uvuvi ili kuwawezesha wavuvi wengi kuvinunua.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa kundi la Usimamizi wa Ufuo kwenye eneo la Suba Kusini William Onditi, alisema fedha hizo pia zinafaa kutumika kukamilisha ujenzi wa soko la samaki ambalo liliahidiwa na Rais William Ruto.

Onditi aliitaka serikali kujenga soko hilo katika mwaka mpya wa kifedha unaoanza mwezi ujao.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *