Wauza pombe Laikipia walalamikia sheria mpya

Dismas Otuke
1 Min Read

Wafanyabiashara katika kaunti ya Laikipia wamelalamikia sheria mpya iliyopendekezwa kudhibiti pombe katika kaunti hiyo.

Wamiliki wa baa na maeneo mengine ya kuuza pombe wamesema sheria zilizopitishwa na bunge la kaunti hiyo ili kudhibiti uuzaji na unywaji pombe huenda zikaathiri wawekezaji katika sekta hiyo.

Mswada huo unalenga kufutilia mbali baadhi ya leseni zilizotolewa awali kama kuuza “mtura” katika maeneo ya burudani.

Pia sheria hiyo mpya inalenga kupunguza idadi ya vilabu vinavyopewa leseni kuuza pombe kwenye kaunti hiyo.

Kulingana na mwenyekiti wa Wamiliki wa baa Benson Kalama, iwapo sheria hiyo itapitishwa, huenda ikachangia kwa vijana zaidi ya 20,000 kupoteza ajira kwenye kaunti hiyo, akiongoza kuwa haelewi umuhimu wa sheria hizo kali ilhali hawausiki katika uuzaji wa pombe haramu.

TAGGED:
Share This Article