Watu wawili wamehukumiwa kifo nchini Iran kwa madai ya kuchoma Quran na kumtusi mtume wa waislamu, kwa mujibu wa mahakama moja nchini humo.
Yousef Mehrad na Sadrollah Fazeli-Zare walikuwa na akaunti za mitandao za kijamii walizozitumia kutukana Mungu na kudhalilisha utakatifu, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la mahakama.
Wakili wa Mehdad alisisitiza kwamba mteja wake hakuwa na hatia na hukumu hiyo si ya haki. Mizan ilisema Yousef Mehrad na Sadrollah Fazeli-Zare walinyongwa katika gereza la Arak kati kati mwa nchi ya Iran leo asubuhi.
Mwaka wa 2021, mahakama ya uhalifu ya Arak iliwapata na hatia wawili hao na kutoa hukumu ya kifo.
Pia walipewa hukumu ya miaka sita gerezani kwa kubuni vikundi dhidi ya usalama wa kitaifa.