Takriban waganga 4000 Kaunti ya kilifi sasa wanaitaka serikali kuu na ile ya kaunti ya kilifi kuwatambua sawia na kuwapa vibali waganga wote nchini ambao wanatibu wagonjwa kupitia tiba asili
Baadhi ya waganga hao ambao wamekongamana katika kituo cha kitamadani cha Gongoni kule Magarini wanasema kuwa wana uwezo wa kutibu magonjwa mbali mbali ambayo baadhi ya madaktari waliohitimu wameshindwa kuyatibu.
Wakizungumza baada ya kuzindua kituo chao cha utafiti wa tiba asilia wakiongozwa na Tsuma Nzai wansema kuwa serikali kupitia wizara ya afya na utamaduni inafaa kuwatambua na kufanya kazi na madaktar ili kutoa huduma za afya hasa mashinani.
Aidha wanasema kuwa kituo hicho kitasaidia pakubwa katika kufanya utafiti wa miti asilia itakayotumika kwa matibabu .
Wanasema kuwa baadhi yao wamekua wakiishi kwa hofu kutokana na dhana kuwa waganga wanashiriki uchawi hivyo wakitaka serikal kuwatambua.
Hata hivyo baadhi ya madaktar akiwemo Eddy Chengo ambaye ni Daktar wa kifafa wamekiri kuwa baadhi ya waganga wamehusika zaidi katika Tiba asilia hivyo wapewe vibali na kupewa mazingira bora.