Watu wawili wafariki kwenye ajali Bungoma

Marion Bosire
1 Min Read

Watu wawili wamethibitishwa kufariki kwenye ajali iliyohusisha basi la bendi ya polisi, lori na pikipiki katika eneo la Matete kaunti ya Bungoma.

Wengine wanane ambao wote ni wanachama wa bendi ya polisi walipata majeraha kwenye ajali hiyo na wanasafirishwa kuelekea hospitali ya Eldoret kwa matibabu.

Dereva wa basi ya bendi ya polisi alipinda gari hilo kutoka barabarani kuzuia kugongana ana kwa ana na lori ambalo lilikuwa likigeuzwa barabarani kwa njia isiyofaa lakini kwa bahati mbaya akagonga pikipiki na kuanguka kwenye mtaro.

Share This Article