Watu watatu wamekamatwa na polisi mjini Eldoret kwa kuwahadaa raia kuhusu ajira za ughaibuni.
Watatu hao walinaswa baada ya kuwasafirisha makumi ya vijana hadi mjini Eldoret kutoka vijijini katika kaunti ya Uasin Gishu, wakiwahadaa kuwapa ajira za kufanya kazi nje ya nchi.
Afisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI kaunti ya Uasin Gishu Daniel Muleli alisema baadhi ya vijana walisafirishwa kutoka maeneo ya Ziwa na kuwekwa kwenye mkahawa mmoja mjini Eldoret kabla ya kusafirishwa hadi boma moja eneo la Annex na kuzua taharuki.
Kulingana na Muleli, watatu waliokamatwa walijidai kuwa shirika la kuajiri watu nje ya nchi.
Kwa sasawamezuiliwa ili kusaidia polisi katika uchunguzi.