Watu watano wafariki katika ajali ya barabarani Kajiado

Tom Mathinji
1 Min Read

Watu watano walifariki Alhamisi jioni, huku wengine watatu wakipata majeraha mabaya kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Maili Tisa, Kaunti ya Kajiado.

Ajali hiyo ilitokea wakati gari aina ya Toyota Lexus ilipogongana ana kwa ana na pikipiki iliyokuwa na abiria.

Watu watatu waliokuwa ndani ya gari hilo walifariki papo hapo, huku wawili wakifariki walipokuwa wakitibiwa katika hospitali ya Namanga.

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa polisi Kaunti ndogo ya Oloililai Hassan Elena, alisema waliokuwa kwa pikipiki walipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kajiado ambako wanapokea matibabu.

Elena alitoa wito kwa waendeshaji magari katika barabara hiyo kuwa makini zaidi ili kupunguza ajali za barabarani.

Miili ya waliofariki ilipelekwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya rufaa ya Kajiado.

Website |  + posts
Share This Article