Watu wanne wamethibitishwa kufariki na wengine wanane wanapokea matibabu katika vituo kadhaa vya afya kaunti ya Migori, baada ya kubugia pombe inayoshukiwa kuwa na sumu.
Wanne hao wanaojumuisha muuzaji wa pombe hiyo, walifariki walipokuwa wakipokea matibabu katika hospitali ya Samjomen Kuria Magharibi walikopelekwa na wasamaria wema.
Kulingana na wakazi, waliofariki walikuwa miongoni mwa kundi la watu waliokuwa wakibugia pombe usiku kucha, kabla ya kukumbwa na matatizo ya kupumua na kuongea.
Aidha wakazi hao walitoa wito kwa viongozi wa serikali kufanya msako mkali dhidi ya pombe haramu ambayo imekithiri katika eneo hilo.