Watu sita wauawa kwa kudungwa kisu nchini China

Tom Mathinji
1 Min Read

Watu sita wakiwemo watoto watatu, wameuawa na mwingine kujeruhiwa katika kisa cha kudungwa visu katika shule moja ya chekechea, katika mkoa wa Guangdong kusini mashariki mwa China.

Wahanga wengine ni mwalimu mmoja na wazazi wawili kwa mujibu wa afisa mmoja wa serikali eneo hilo.

Polisi wamesema wamemtia mbaroni mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 25 katika mji wa Lianhiang.

Tukio hilo lilitokea muda tu wazazi walipokuwa wakiwapeleka watoto wao shuleni kwa masomo ya msimu wa joto unaoendela.

Silaha zimepigwa marufuku nchini China lakini taifa hilo limeshuhudia visa vya watu kudungwa visu katika siku za hivi karibuni.

Katika nyingi ya visa hivyo, washambulizi wamekuwa wanaume wenye chuki dhidi ya jamii.

Miendendo kama hiyo imeshuhudiwa katika mauaji ya halaiki katika mataifa mengine kama vile Marekani na Japan.

Wataalam nchini China hata hivyo wamesema huenda kukawa na sababau nyingine ya ongezeko la matukio ya visa hivyo nchini humo.

Kwa kuhofia mashambulizi mengine ya aina hiyo, Beijing imevizuia vyombo vya habari dhidi ya kuchapisha maelezo kamili ya tukio la leo katika shule hiyo ya chekechea.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *