Watu saba wahofiwa kufa baada ya kusombwa na mafuriko Makueni

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu saba wanahofiwa kufariki katika kaunti ya Makueni, baada ya kusombwa na mafuriko yanayotokana na mvua kubwa.

Yamkini saba hao walisombwa walipojaribu kuvuka mto Muuoni uliokuwa umevunja kingo Alhamisi usiku waliposombwa.

Kulingana Chifu wa eneo hilo Norman Musyoki, saba hao walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano uliongozwa na mkewe Rais, Rachel Ruto katika uwanja wa Kasarani walipokumbana na kifo.

Mkewe Rais ametuma risala za rambirambi kwa familia za walioathiriwa na mkasa huo akisema anasimama nao wakati huu mgumu wa majonzi.

Share This Article