Watu 7 wafariki kwenye ajali barabara ya Nairobi-Nakuru

Martin Mwanje & Ephantus Githua
1 Min Read

Watu 7 wamefariki katika ajali ya barabarani iliyotokea kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru. 

Watu wengine walijeruhiwa wakati wa ajali hiyo iliyotokea kwenye makutano ya Kamandura hiyo.

Ajali hiyo ilitokea baada ya matatu ya Kijabe Line Sacco walimokuwa wakisafiria kubingiria mara kadhaa baada ya dereva kuripotiwa kupoteza mwelekeo.

Ajali hiyo ilitokea chini ya saa 12 baada ya watu wengine watano kufariki umbali wa chini ya kilomomita 3 kutoka eneo la ajali ya hivi punde.

Ajali ya awali ilihusisha gari la binafsi la kubeba watu 14.

Martin Mwanje & Ephantus Githua
+ posts
Share This Article