Watu 60 wauawa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani Sudan

Tom Mathinji and BBC
1 Min Read
Watu 60 wafariki kwenye shambulizi la ndege zisizo na rubani Sudan.

Takriban watu 60 wameuawa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani katika eneo la watu waliokimbia makazi yao huko El-Fasher, mji uliozingirwa na uliokaribu kuporomoka nchini Sudan.

Kamati ya upinzani ya El-Fasher, inayoundwa na raia na wanaharakati wa eneo hilo, iliarifu kuwa kikosi cha Sudan (RSF) kilitekeleza mashambulizi mawili ya ndege zisizokuwa na rubani na mizinga nane.

“Watoto, wanawake na wazee waliuawa huku wengine wakiteketea kwa moto kabisa,” taarifa ya kundi hilo ilisema.

Mashuhuda walielezea matukio hayo ya kuogofya wakati waokoaji wakiondoa miili kutoka kwenye vifusi.

Hospitali ambazo tayari zinakabiliwa na miezi kadhaa ya kuzingirwa zimezidiwa, huku madaktari wakiwatibu majeruhi kwenye sakafu na viambaza.

RSF imezingira El-Fasher kwa muda wa miezi 17 sasa, katika jaribio la kuchukua udhibiti wa ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan huko Darfur.

Kwa mujibu wa kamati hiyo hali katika eneo la El-Fasher “imevuka maafa na mauaji ya halaiki”.

Sudan imekumbwa na mzozo tangu mwaka 2023, baada ya makamanda wakuu wa jeshi la RSF na Sudan kutoelewana na kuzuka mzozo mkali wa madaraka na kusababisha moja ya mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu

Website |  + posts
Share This Article