Watu watano wamefariki katika ajali ya barabarani, ilyohusisha magari matatu katika eneo la Kibirigwi kwenye barabara ya kutoka Sagana kuelekea Karatina kaunti ya Kirinyaga.
Kulingana na naibu kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Kirinyaga Magharibi Moses Koskei, dereva wa lori hilo lililokuwa likielekea Sagana likisafirisa magunia ya mahindi,alishindwa kulidhibiti ambapo lilipoteza mwelekeo na kugonga magari mawili ya kibinafsi yaliyokuwa yakielekea Karatina.
“Watu watano walifariki pao hapo, huku idadi isiyojulikana ya watu wengine wakijeruhiwa na kupelekwa katika hospitali tofauti katika eneo hilo,” alisema kamanda huyo wa polisi.
Lori hilo lilipinduka, magunia ya mahindi yakitapakaa barabarani, huku baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakipora mahindi hayo.
Afisa huyo wa polisi alisema uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo.