Tume ya haki za kibinadamu KNHCR imefichua kuwa idadi ya waliofariki nchini kutokana na maandano ya vijana wa Gen Z imefikia 39.
Kwa mjibu wa takwimu za KNHCR watu wengine 361 wamejeruhiwa, huku wengine 32 wakitekwa Nyara kwa njia za kutatanisha na 627 wakikamatwa na polisi.
Maandamano hayo ambayo yamedumu kwa majuma mawili pia yamesababisha uharibifu wa mali.
Watu 39 waliofariki wanajumuisha 17 kutoka kaunti ya Nairobi, wanne kaunti ya Uasin Gishu watatu kaunti za Nakuru ,Kajiado, na Mombasa.
Kaunti za Kisii na Kakamega zimenakili vifo wawili kila moja.
Narok ,Laikipia,Siaya, Kiambu na Nandi zimeripoti kifo kimoja kila moja.