Waokoaji wameopoa mili 26 ya watu walioangamia kutokana na mafuriko nchini Korea Kusini.
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo imesabaisha mafuriko ambayo yameleta hasara kubwa ikiwemo kukatizwa kwa nvuvu za umeme na maporomoko ya ardhi.
Watu wengine 10 hawajulikani waliko huku ikiaminika kuwa huenda wengine zaidi wamefunikwa kwenye barabara moja ya kupita chini ya ardhi iliyo ya kina cha mita 685 na yakisiwa zaidi yamagari 15 huenda yamefunikwa chini ya ardhi.