Watu 228 wafariki kutokana na mafuriko

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya watu 228 wamefariki kote nchini kutokana na athari za mafuriko ya mvua baada ya wengine 9 kuaga dunia, ndani ya saa 24 zilizopita wakiwemo watu wazima 7 na watoto wawili.

Kulingana na taarifa ya msemaji wa serikali kwa vyombo vya Habari Isaack Mwaura ,watu 164 wajeruhiwa huku wengine 72 wakiwa hawajulikani waliko, na wengine 212,630 wakilazimika kuhama makwao kutokana na mafuriko.

Katika mkasa wa maporomoko ya ardhi watu 52 wamefariki eneo la Mahi Mahiu, huku hatma ya  wengine 51 ikiwa haijulikani wakati ambapo maafisa 400 wa NYS na wanajeshi wa KDF  151 wakiendeleza  shughuli ya kutafuta miili.

Katika kaunti ya Nairobi jumla ya watu 163,210  waliokuwa wakiishi karibu na mito wamehamishwa.

Taarifa hiyo pia imeelezea kuwa mvua kubwa inatarajiwa maeneo mengi nchini baina ya  Jumapili,Jumatatu na Jumanne .

Share This Article