Watu 15 wauawa katika mashambulizi Burkina Faso

Martin Mwanje
1 Min Read
Watu 15, wengi wao raia, waliuawa katika “mashambulizi ya wakati mmoja” mwishoni mwa wiki mashariki mwa Burkina Faso, vyanzo vya usalama na vya nchi hiyo viliiambia AFP leo Jumanne. 

Taifa hilo la Afrika Magharibi linahangaika kukabiliana na uasi wa jihadi uliotokea nchi jirani ya Mali mnamo mwaka 2015 na kuacha raia zaidi ya 17,000 na wanajeshi wakiwa wamefariki.

Mamilioni ya watu waliachwa bila makazi.

Katika vurugu za hivi punde, watu 15, wakiwemo wanajeshi wasaidizi watatu, waliuawa Jumamosi iliyopita katika “mashambulizi ya wakati mmoja na kuoanisha” huko Diapaga, mji mkuu uliopo katika jimbo la mashariki la Tapoa, mkazi aliiambia AFP.

Kondia Pierre Yonli, msemaji wa shirika moja la kijamii la kanda hiyo alithibitisha taarifa hizo akiongeza kuwa shule, masoko na huduma za umma zilisitishwa kanda hiyo leo Jumanne kuwaenzi waathiriwa waliozikwa juzi Jumapili katika makaburi ya manispaa ya Diapaga.

Chanzo cha usalama kilisema jeshi linatekeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Share This Article