Maafisa wa uokoaji nchini Sierra Leone wanaendelea na shughuli ya kuwatafuta manusura zaidi baada ya jengo la ghorofa saba kuporomoka katika mji mkuu Freetown na kusababisha vifo vya takriban watu 10.
Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Majanga la nchi hiyo ya Afrika Magharibi (NDMA) lilisema watu saba wameokolewa kufikia sasa, lakini “watu zaidi wamenaswa”.
Iliongeza kuwa baadhi ya wale waliokuwa kwenye vifusi “wameweza kuwasiliana na jamaa zao” kwa mujibu wa waokoaji.
Jengo hilo lililo mashariki mwa Freetown liliporomoka kati ya saa tano na saa sita majira ya ndani (12:00 na 13:00 BST) siku ya Jumatatu, NDMA ilisema.
Mkazi wa eneo hilo Mohamed Camara aliangua kilio alipoambia shirika la habari la AFP kwamba mke wake na watoto watatu walikuwa wamenasa kwenye vifusi
Jengo hilo lilitumika kwa madhumuni ya makazi na biashara, kulingana na tathmini za awali zilizofanywa na NDMA.
Mkuu wa shirika hilo Brima Sesay alisisitiza umuhimu wa “kuhamasisha umma kuhusu hatari zinazohusiana na kuwatumia wakandarasi wasio na ujenzi”.
Sierra Leone ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, na mara nyingi majengo hujengwa kwa vifaa vya hali duni.