Watatu wafariki kufuatia ajali ya barabarani Murang’a

Kbc Digital
1 Min Read
Ajali iliyotokea kwenye barabara ya Murang'a-Kenol na kuua watu watatu

Watu watatu walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na ajali ya barabarani iliyohusisha matatu mbili kwenye barabara kuu ya Murang’a-Kenol leo Jumatatu asubuhi. 

Kwa mujibu wa manusura na mashuhuda, matatu ya Murang’a Shuttle iliyokuwa ikielekea Nairobi iligongana ana kwa ana na matatu ya chama cha ushirika cha Nakkons iliyokuwa ikielekea upande wa Murang’a.

Wakati wa tukio hilo, abiria 24 waliokuwa kwenye magari hayo mawili ya umma walipata majeraha mabaya na kupelekwa katika hospitali ya Murang’a Level 5 kwa ajili ya matibabu.

Ajali hiyo ilithibitishwa na kamanda wa tarafiki wa Murang’a Kennedy Muthamia ambaye alisema abiria wawili wa kike walifariki papo hapo.

Abiria mwengine wa kiume alifariki kabla ya kufikishwa hospitalini.

Kumekuwa na ongezeko la ajali za barabarani humu nchini kiasi kwamba wadau katika sekta hiyo wametaka ajali hizo kutangazwa kuwa janga la kitaifa.

Taarifa ya Wambui Mwangi 

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *