Watatu wafariki baada ya kuangukiwa na ndege Malindi

Ndege hiyo Aina ya Cesna ilikua na wanafunzi watatu wakati ilipata hitilafu angani na kuanguka mkabala na barabara ya kutoka Malindi kuelekea Kilifi.

Marion Bosire
1 Min Read

Watu watatu wamefariki papo hapo baada ya kuangukiwa na ndege katika eneo la Kwa chocha huko malindi kaunti ya kilifi.

Ndege hiyo Aina ya Cesna ilikua na wanafunzi watatu wakati ilipata hitilafu angani na kuanguka mkabala na barabara ya kutoka Malindi kuelekea Kilifi.

Mmoja kati ya waliofariki ameungua kiasi cha kutotambulika kufuatia kuanguka kwa ndege hiyo na kushika moto huku wengine wawili waliofariki wakiwa mhudumu wa bodaboda ambaye alikua amebeba abiria mwanamke.

Mkufunzi wa ndege hiyo pamoja na wenzake wawili wameokolewa na kukimbizwa katika hospitali ya kibinafsi ya Tawfiq ambapo wanaendelea kupokea matibabu.

Polisi wamefika katika eneo la tukio na kuanzisha uchunguzi wa ajali hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *