Watatu waangamia kwenye ajali ya barabarani Kilifi

Dismas Otuke
1 Min Read
Kaka wawili wauawa Kakamega.

Watu wapatao watatu wamefariki wakati wa sikukuu ya Krismasi katika kaunti ya Kilifi.

Hii ni baada ya dereva wa lori kupoteza mwelekeo na kuwagonga watatu hao katika barabara yenye idadi kubwa ya watu ya Mariakani-Kaloleni.

Kulingana na taarifa za poisi, ajali hiyo imetokaea saa kumi na moja asubuhi ambapo pia watembeaji wengine watatu wa miguu walijeruhiwa.

Ingawa polisi wameanzisha uchunguzi, yamkini dereva wa lori hilo lililokuwa limebeba mchanga alipoteza mwelekeo akiwa kwenye mteremko baada ya gurudumu kupasuka na kugonga magari kadhaa yaliyokuwa yameegeshwa kando.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *