Watu watano walifariki papo hapo na wengine 10 wakajeruhiwa, kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha matatu ya abiria 14 katika eneo la Londiani, kaunti ya Kericho mapema Jumamosi.
Ajali hiyo ilitokea Jumamosi alfajiri, wakati matatu hiyo ipogongana na trela kwenye barabara kuu ya Kericho.
Kulingana na ripoti ya Shirika la Msalaba Mwekundu, dereva wa matatu hiyo alipoteza mwelekeo na kuingia kwenye trela na gari hilo kuharibiwa vibaya.
Walioaga dunia walikuwa wanaume wanne na mtoto mmoja huku majeruhi hao 10, wakipelekwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Molo.