Mahakama ya kushughulikia makosa ya ugaidi, imewapata washukiwa wawili na makosa ya kushiriki ugaidi dhidi ya hoteli ya Dusit D2 miaka sita iliyopita, ambapo takriban watu 21 waliuawa.
Kulingana na hukumu ya Lady Justice Diana Kavedza iliyochukua saa nne kusomwa, upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kupitia mashahidi 45, wakiwemo wataalam kubainisha kuwa wawili hao ndio waliopanga shambulizi hilo la kikatili la Aprili 25, 2019.
Justice Diana, katika uamuzi huo wake, alisema ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka unatosha kuwahukumu wawili hao gerezani.
Alisema mshtakiwa wa kwanza Mohammed Abdi Ali na wa pili Hussein Mohamed Abdillie Ali, walikuwa wahusika wakuu katika shambulizi la kigaidi dhidi ya hoteli ya Dusit D2 iliyoko eneo la Riverside.
Hukumu hiyo iliongeza kuwa mshukiwa wa kwanza alitumia vitambulisho kadhaa za wakazi wa Mandera wasio na hatia kufungua kurasa za mtandao wa Facebook na pia kwa kutuma fedha kwa magaidi waliotekeleza shambulizi hilo.
Kwa upande wake mshtakiwa wa pili anadaiwa kutuma pesa na kuwasiliana na waliopanga shambulizi hilo, ambapo alituma zaidi ya shilingi kwa awamu kwa njia ya Mpesa.
Ripoti dhidi ya wawili hao itatayarishwa katika muda wa siku 21 kabla ya kikao cha kuamuliwa kifungo chao kuadaliwa.