Bunge la Taifa litawasaili waliopendekezwa kuwa Makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) siku ya Jumamosi Mei 31,2025.
Hatua hiyo inajiri baada ya Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula kuiagiza kamati ya Haki na Maswala ya Kikatiba (JLAC), kuendelea na zoezi hilo, ambalo lilikuwa limesitishwa na mahakama kwa muda kufuati kesi iliyowalishwa ikikashifu uhalali wa mchakato wa uteuzi wao.
Kamati hiyo sasa itahitajika kuwasilisha ripoti yake ya kuunga mkono au kupinga uteuzi huo bungeni.
Awali Wetangu’ula aliishtumu Idara ya Mahakama kwa kuingilia shughuli za bunge, akikariri uhuru wa kikatiba wa bunge.
Spika huyo alisema kuwa hakuna mtu binafsi,taasisi au asasi ya serikali iliyo na uwezo wa kuagiza na kuzuia bunge kutekeleza majukumu yake
Watakaosailiwa ni pamoja na Erastus Edung Ethekon aliyeteuliwa Mwenyekiti wa IEBC, makamishna wakiwa Anne Nderitu, Moses Mukwana, Mary Karen Sorobit, Hassan Noor, Francis Odhiambo, na Fahima Abdalla.