Maafisa wa polisi kaunti ya Nairobi, wamewakamata washukiwa wawili waliojisingia kuwa maafisa wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI na kuwaibia wakenya fedha zao.
Kulingana na idara ya DCI, wawili hao Nicholas Okoth Owino na David Otieno Odhiambo, walinaswa baada ya kupokea shilingi 200,000 kutoka kwa mwathiriwa, wakijidai kuwa maafisa wa DCI.
Washukiwa hao walidai wanauwezo wa kuharakisha uchunguzi uliokuwa ukiendelea, na kumuingiza mwathiriwa huyo kwenye mtego wao.
“Huku uchunguzi huo ukiendelea, maafisa wa polisi wanashuku kuna uwezekano washukiwa hao wamewapunza waathiriwa wengine,” ilisema idara ya DCI kuptia mtandao wa X.
DCI imetoa wito kwa yeyote huenda alihadaiwa na washukiwa hao kuripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu naye.