Washukiwa wawili wa ujambazi wakamatwa Bomet

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wa ujambazi wakamatwa Bomet.

Maafisa wa polisi wanawazuilia washukiwa wawili wa kundi la majambazi ambalo limekuwa likiwahangaisha wakazi wa kaunti za Bomet, Kericho na Nakuru.

Wawili hao walikamatwa kwenye operesheni inayoendelea ya kuwasaka wahalifu ambao pia wanahusika kwenye wizi wa ki-mtandao.

Kevin Kiplang’at kwa jina lingine Elvis mwenye umri wa miaka 31, na Evan Kiprotich Chirchir kwa jina lingine Protio aliye na umri wa miaka 22 walikamatwa katika sehemu za Mulot na Chepalungu kaunti ya Bomet.

Oparesheni hiyo inayoendelea ikiongozwa na makachero kutoka makao makuu ya DCI inafuatia malalamishi kuhusu kubadilishwa kwa laini za simu na wahalifu walio na kesi mahakamani.

Washukiwa hao wawili wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Litein wakisubiri kutambuliwa na kufikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka ya wizi wa mabavu katika kituo cha polisi tarehe 29 mwezi desemba mwaka uliopita.

Kulingana na DCI, washukiwa hao pia watafikishwa katika vituo vingine vya polisi ambako visa vya wizi wa kieletroniki viliripotiwa ili kubaini kuhusika kwao.

TAGGED:
Share This Article