Washukiwa wawili wa mauaji wakamatwa Busia

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wawili wa mauaji wakamatwa Busia.

Washukiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na kifo cha kutatanisha cha mzee wa umri wa miaka 50 katika kijiji cha  Kamarinyang, Amukura ya kati, eneo bunge la Teso Kusini, kaunti ya Busia.

Mwili wa mzee huyo ulipatikana ukining’inia kwenye mti wa maparachichi nyumbani kwake, kisa ambacho awali kilionekana kuwa cha kujitoa uhai.

Akizungumza na wanahabari, mwana wa kiume wa mzee huyo Benson Karani, alisema walipokea simu kutoka kwa ndugu wao mdogo kuwafahamisha kuwa babayao amejitoa uhai.

Hata hivyo, wasiwasi uliibuka baada ya familia kuutazama mwili wa babayao, na kutoa wito wa uchunguzi wa kina. Familia hiyo sasa inatoa wito kwa serikali kuisadia wanapojiandaa kumzika mpendwa wao.

Kulingana na Chrispinus Omusugu, ambaye ni kaka wa marehemu, uchunguzi wa maiti ulibaini kuwa mwili huo ulikuwa na majeraha, ikiwa ni pamoja na mbavu nne kujunvika, jeraha kwa mguu na alama za majeraha shingoni, ishara kwamba alinyongwa na wala sio kujitia kitanzi.

Blanketi mbili zilizokuwa zimeloa damu, shoka na nyundo zinazoaminika kutumika katika kisa hicho, zilipatikana katika eneo hilo.

TAGGED:
Share This Article